be the first to know..
MANCHESTER UNITED, WABABE WA SOKA ULIMWENGUNI
MABINGWA wa Ligi Kuu ya England, Manchester United wametangazwa kuwa klabu ya michezo yenye thamani kubwa ulimwenguni.
United au Mashetani Wekundu wanaongoza orodha hiyo ya klabu 50 za michezo mbalimbali duniani ikiwa na rasilimali zenye thamani ya pauni1.165 bilioni.Klabu hiyo imezipiku klabu mbalimbali za michezo za Marekani zikiwamo Dallas Cowboys na New York Yankees.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, tathmini hiyo imezingatia kikosi, uwanja, mapato na udhamini ambao kila klabu inao kwa sasa. Jarida hilo linaeleza kuwa hizo ni habari njema kwa wanandugu wa ukoo wa Glazer wanaomiliki klabu hiyo ambayo waliinunua kwa pauni 790 milioni mwaka 2005.
Hata hivyo, familia hiyo imejikuta ikiingia deni la pauni 500 milioni katika uendeshaji wa klabu hiyo.
Mapato ya matangazo yameiingizia United kiasi kikubwa che fedha, ambacho ni pauni 80 milioni.
Pia, mkataba wa miaka minne wa udhamini wa jezi na Kampuni ya Aon na mkataba wa miaka 13 na Kampuni ya Nike umeingiza pauni 300m .
Kwa upande wake, klabu ya Real Madrid ya Hispania ambayo ilikuwa ikishika nafasi ya pili katika orodha hiyo imeporomoka na kushika nafasi ya tano ikiwa na rasilimali zenye thamani ya pauni 900m. Lakini, pengine klabu ambayo mashabiki wake watakuwa wenye furaha ni Arsenal, ambayo inashika nafasi ya saba ikiwa na rasilimali za pauni 740m.
Chelsea, chini ya tajiri Roman Abramovich, inashika nafasi ya 46 katika orodha hiyo, ambayo timu za soka ndizo zinaongoza katika orodha zikiwamo Bayern Munich (19), AC Milan (34) na Juventus (49).
Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kuona Barcelona, ambayo kwa sasa inasemekana kuwa klabu bora duniani, ikiwa ya 26 katika orodha hiyo kwa rasilimali za pauni 606m.
Nafasi 10 za kwanza ni kama ifuatavyo:
1. Man United - Pauni 1.165bilioni
2. Dallas Cowboys- Pauni 1.13bn
3. New York Yankees- Pauni1.06bn
4. Washington Redskins- Pauni 960m
5. Real Madrid- Pauni 900m
6. New England Patriots- Pauni 850m
7. Arsenal- Pauni 740m
8. New York Giants- Pauni 734m
9. Houstan Texans- Pauni727m
10. New York Jets- Pauni 708m
Ongezeko kubwa la idadi ya watu nchini India imewalazimu maafisa wa Afya kuanza kampeni mpya ya mpango wa uzazi.
Serikali inawasiwasi kuhusu idadi kubwa ya watu
Wanaokubali watapokea zawadi ya gari lipya miongoni mwa zawadi nyingine.
Tata nano, ndio gari lenya bei rahisi sana duniani lakini kulingana na kampeni hiyo, bila shaka kuna uwezekano likawa maarufu zaidi nchini India katika siku chache zijazo.
Dakatri Sitaram Sharma anatazamia kuwa huenda gari hilo likawa kishawishi tosha kwa wakazi wa jimbo la Jhunjunu kujitokeza kufungwa kizazi.
Lengo la Daktari Sharma ni kuwa jumla ya wanawake na wanaume elfu 20 watajitokeza kufungwa kizazi.
Kwa taarifa yako, gari sio zawadi tu itakayotolewa kwenye kampeni hiyo. Watakao fika watapewa piki piki, televisheni na vifaa vya kisasa vya kusagia vyakula.
Mpango huo hauja lenga tuu wakaazi wa jimbo hilo ambalo mara nyingi linakabiliwa na ukame.
Serikali ya India imekuwa ikitatizika na idadi ya raia wake ambayo inakuwa kwa kasi sana.
Hofu za utawala nchini India ni kuwa ifikiapo mwaka wa 2030, heunda idadi ya watu walioko nchini humo ikazidi ile ya wachina.
Hata hivyo hakuna uhakika kuwa kampeni hii itaungwa mkono kote nchini India.
Mwaka wa 70 ilipojaribiwa, maelfu ya watu walijotekeza kisha serikali ikashindwa kutimiza ahadi zake kitu kilicho wachukiza wengi ambao walidai kuwa serikali ilikuwa imewalaghai...


