Thursday, June 9, 2011

KIJANA AUZA FIGO YAKE KWA FEDHA ZA ANASA

Kijana mmoja nchini Uchina alikuwa akitamani sana kupata kifaa kipya cha mawasiliano aina ya iPad 2 kiasi kwamba aliamua kuuza figo yake ili anunue kifaa hicho.
iPad ni kifaa cha kisasa ambacho kinaweza kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuhifadhi muziki na pia kurambaza kwenye mtandao.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 aliyejulikana kwa jina moja tu la Zheng alikiri kwa mama yake kuwa aliamua kuuza figo yake baada ya kuona tangazo la mtu anayetaka kununua figo kwa dola elfu mbli za kimarekani.
"Nilitamani sana kuwa na iPad 2 lakini sikuwa na pesa" amesema kijana Zhang akizungumza na kituo cha televisheni cha Shenzen, katika jimbo la Guangdong. Kijana Zheng aliporudi nyumbani mama yake aligundua mara moja.
"Aliporudi, alikuwa na laptop mpya na iPad mpya" amesema mama yake, huku akionesha kidonda ambapo mwanae alifanyiwa upasuaji kutoa figo. "Nilitaka kujua alipata wapi pesa za kununua vitu hivyo vya gharama kubwa, na ndipo akakiri kuwa ameuza figo yake moja" amesema mama huyo.
Simu za iPhone na kifaa cha iPad ambazo hutengenezwa na kampuni ya Apple ni maarufu sana hasa kwa vijana kuonesha ufahari wao nchini Uchina.

kwa tathimini ya fasta, , mimi binafsi yangu naweza kumufananisha kijana ZHENG na JAMBAZI kwa sababu jambazi ndie anafanya kitu hata cha kuya risk maisha yake ilimuradi apate hitaji lake. ni kweli vijana wa leo wote tunahitaji vitu vizuri na vya bei kwasababu ya kile kinachoitwa ' utandawazi' alakini tukumbuke starehe ni gharama hivyo yatupasa kujishughulisha na sio kuji 'assasinate'.

                    Muga Ze great!!