Tuesday, August 9, 2011

uganda yanufaika na sukari ya kagera

BE THE FIRST TO KNOW, FROM THIS CUTTING EDGE PLATFORM;

BEI kubwa ya sukari imezidi kuvuruga Mkoa wa Kagera, baada ya kuingiliwa na wafanyabiashara kutoka Uganda, huku ikipanda hadi Sh2,400 kwa kilo tofauti na Sh1,700 iliyotangazwa na Serikali.Uchunguzi uliofanywa kwa baadhi ya miji ya kagera kama Bukoba na karagwe, umebaini wafanyabiashara kutoka Uganda wameteka soko la sukari na kusababisha kupanda kutokana na mahitaji makubwa yanayodaiwa kuwapo nchini humo(demand kuwa kuwa zaid ya supply).

Katika maduka mbalimbali mjini Bukoba, licha ya bei ya sukari kupanda huku Serikali ikishindwa kusimamia agizo lake la kuteremsha bei, baadhi ya wafanyabiashara wa maduka wanalalamikia kukosa bidhaa hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara walidai kuna ukiritimba katika usambazaji sukari, msambazaji ni mmoja ambaye anahusishwa na kuadimika kwa bidhaa hiyo kwa madai ya kuiuza kwa wafanyabiashara wa Uganda, ili kupata faida kubwa.

kwa upande wa karagwe, wafanya biashara wadogo wadogo hususani wale wa maduka wanalazimika kulangua sukari toka Uganda. wafanyabiashara hao ni pamoja na wale wa murongo, Rugasha, kibingo na hata kaisho.
Duka la bwana Kanini hapo kikagati uganda,ambalo ni msambazaji mkubwa wa bidhaa za duka kwa Watanzania wauza duka.


Akizungumzia matatizo ya kupanda holela kwa bei ya sukari mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mohamed Babu, alikiri bei ya sukari kupanda kwa kasi mkoani hapa na kwamba, tayari amepewa taarifa za kuwapo kwa wafanyabiashara wa Uganda.Hata hivyo, Babu alikitetea Kiwanda cha Sukari Kagera na msambazaji wake kuwa, hawahusiki na upandaji sukari na kudai kuwa, hakuna sababu ya wafanyabiashara kupandisha bei.

Licha ya kudai kuwa serikali ina mkono mrefu wa kudhibiti upandaji bidhaa hiyo, kwa miezi kadhaa tangu kutolewa kwa bei elekezi, hakuna mabadiliko yaliyofanywa kushuka bei.

Badala yake, Babu alisema Serikali haiwezi kudhibiti upandaji sukari hadi maeneo ya vijijini na kuwaomba wananchi kutoa taarifa, ili ichukue hatua kwa wanaokaidi maelekezo ya bei halali.

Pia, taarifa kutoka Wilaya ya Missenyi ambayo ipo kilomita 18 kufika mpaka wa Mutukula, zilidai wafanyabiashara kutoka Uganda wamechangia kupanda kwa bidhaa hiyo kati ya Sh2,500 hadi Sh3,000.