Monday, August 1, 2011

BE THE FIRST TO KNOW, FROM THIS CUTTING EDGE PLATFORM;

Man United yaichapa Barca 2-1
Monday, 01 August 2011 08:47

WASHINGTON, Marekani
MSHAMBULIAJI Michael Owen alifunga bao dakika ya 76 na kuisaidia Manchester United kulipa kisasi kwa kuichapa Barcelona 2-1kwenye mchezo wa kirafiki uliofaninishwa na marudio ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Nani alifunga bao la kwanza dakika ya 22 kwa mabingwa hao wa England, Manchester United ambao walipokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa vigogo hao wa Hispania kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Wembley mwezi Mei.

Shukrani kwa klabu hizo kukubali kucheza mechi hiyo kwenye Uwanja wa FedEx Field jijini Washington nyumbani kwa timu ya NFL 'Redskins' uliochukua mashabiki 81,807, wakiwa ni mashabiki wengi zaidi kuwai kushudia soka hapo Washington DC.

Tom Cleverley alitegeneza bao la Owen, kwa kuiba pasi ya Sergio Busquets aliyokuwa akimpigia Seydou Keita na ilipokuwa ikielekea goli ilimkuta Owen, ambaye alipitisha mpira juu ya kipa wa Barcelona, Victor Valdes.

Dakika sita kabla Thiago Alcantara alisawazisha kwa shuti kali akimalizia mpira wa kona uliopigwa na winga Carlos Carmona.

Ushindi huo umeifanya Manchester United kumaliza ziara ya Marekani kwa kushinda mechi zote tano za kirafiki.

"Ilikuwa ni mechi ya kufa au kupona," alisema kocha msaidizi wa United, Mick Phelan. "Ni mechi muhimu kwa wachezaji kwa jinsi walivyojituma na kupata matokeo mazuri dhidi ya timu bora.

"Tunawachezaji wengi chipukizi na wamethibisha kwamba wanaweza kucheza kwa kiwango cha juu."

Barcelona, ikicheza bila ya mwanasoka bora wa dunia, Lionel Messi pamoja na Daniel Alves, Javier Mascherano na Alexis Sanchez kwenye ziara hiyo ya Marekani, watacheza mechi nyingine jijini Miami dhidi ya Chivas Guadalajara ya Mexico ikiwa ni mechi yao ya pili.

"Tunajiamini vya kutosha," alisema Guardiola akiwa kwenye maandalizi yake kwa ajili ya msimu mpya wa Hispania utakaonza mwishoni mwa mwezi. "Ni vigumu kujiamini ukiwa na wachezaji kama hawa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking