Monday, July 18, 2011

be the first to know.
MZUNGU MSOMI KAGEUKIA UGANGA

WA KIENYEJI

Bwana mmoja aliyekuwa akifanya kazi benki pale Uingereza, ameamua kuacha kazi hiyo na kuwa mganga wa kienyeji Afrika Kusini.

Bwana huyo Thomas Heathfield alipatiwa mafunzo ya kuwa mganga wa kienyeji, ikiwa ni pamoja na kukaa siku tatu bila kulala, na kucheza usiku, kila siku pamoja na kunywa damu ya mbuzi.

Bwana huyo pia alipitia mitihani mbalimbali, ambayo hyaijatajwa, ili kuthibitisha kuwa anafaa kuwa sangoma.

Heathfield alipatiwa jina la Gogo Mndawe baada ya kuweza kujifunza kuzungumza ki- sisiswati na pia kufaulu mitihani kwa miezi mitatu katika kijiji kimoja kilichopo katika jimbo la Mpumalanga, Afrika Kusini.

"Baba yangu na mama yangu walikuja siku nilipomaliza mafunzo, pamoja na wanakijiji kama mia mbili hivi" amesema bwana Heathfield akikaririwa na gazeti la The Sun.

Bwana huyo amesema alipata mwamko wa kiroho, uliomfanya aache kazi yake yenye kipato kikubwa