Friday, July 22, 2011

be the first to know..
TATIZO LA UMEME NCHINI, FAIDA KWA NCHI JIRANI;
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika Mashariki ambayo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikikabiliwa na tatizo sugu la umeme.

Maelezo yanayotolewa na serikali ya Tanzania pamoja na shirika la Umeme Tanzania Tanesco ni kuwa ukame ndio chanzo kikuu cha matatizo ya umeme nchini hapa.

Kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania ndio inayoongoza kwa kukumbwa na uhaba wa umeme mara kwa mara, licha ya kuwa nchi nyingine za Jumuiya hiyo kama Burundi na Uganda zimekuwa zikikabiliwa na upungufu wa umeme.

kwa upande mwingine, serikali ya tanzania haina budi kulaumiwa kwani ni kama vile imeyatelekeza baadhi ya maeneo ya nchi. mfano, katika mkowa wa Kagera hususani mashariki, mpakani mwa border ambayo ni kiunganishi cha nchi tatu Uganda, Tanzania na rwanda. Mrongo-kikagati border, inaziunganisha nchi hizo tatu na kurahisisha mwingiliano ki biashara kupitia Daraja kubwa la kivukio mto kagera lilojengwa kwa nguvu za Wananchi wa halimashauri ya karagwe kupitia uhisani wa wa Dutch kwa milion zipatazo 750/=. alakini cha kusikitisha, ni kwamba upande wa uganda umeendelea zaidi ya Tanzania hivyo kuwasawishi watanzania wa mpakani kufanyia biashara zao uganda. kikagati ambayo ndo pua na mdomo na mrongo ina umeme wa masaa 24, mrongo kiza kitupu, watu wanaishia kutumia tochi za mchina. je, serikali imeshindwa nini kuuvuta ule umeme wa kikagati na kuwanufaisha wa tanzania waishio karibu na mpaka. nadhani serikari ikiwa serious Mrongo na vijiji jirani kama rugasha, kibingo, na hata Kaisho hakutakuwepo tatizo la umeme na Biashara zitabaki nchini badala ya kukimbilia Uganda.



mji wa kikagati umeendelea..

uganda wanafaidi mpaka kwa kuutumia vizuri uzembe wa serikari ya Tanzania.
mwanachi mpakani upande wa tanzania akinyoa kwa kutumia umeme wa betri;