Sunday, July 17, 2011

be the first to know..
MANCHESTER UNITED, WABABE WA SOKA ULIMWENGUNI

MABINGWA wa Ligi Kuu ya England, Manchester United wametangazwa kuwa klabu ya michezo yenye thamani kubwa ulimwenguni.

United au Mashetani Wekundu wanaongoza orodha hiyo ya klabu 50 za michezo mbalimbali duniani ikiwa na rasilimali zenye thamani ya pauni1.165 bilioni.Klabu hiyo imezipiku klabu mbalimbali za michezo za Marekani zikiwamo Dallas Cowboys na New York Yankees.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, tathmini hiyo imezingatia kikosi, uwanja, mapato na udhamini ambao kila klabu inao kwa sasa. Jarida hilo linaeleza kuwa hizo ni habari njema kwa wanandugu wa ukoo wa Glazer wanaomiliki klabu hiyo ambayo waliinunua kwa pauni 790 milioni mwaka 2005.
Hata hivyo, familia hiyo imejikuta ikiingia deni la pauni 500 milioni katika uendeshaji wa klabu hiyo.

Mapato ya matangazo yameiingizia United kiasi kikubwa che fedha, ambacho ni pauni 80 milioni.

Pia, mkataba wa miaka minne wa udhamini wa jezi na Kampuni ya Aon na mkataba wa miaka 13 na Kampuni ya Nike umeingiza pauni 300m .

Kwa upande wake, klabu ya Real Madrid ya Hispania ambayo ilikuwa ikishika nafasi ya pili katika orodha hiyo imeporomoka na kushika nafasi ya tano ikiwa na rasilimali zenye thamani ya pauni 900m. Lakini, pengine klabu ambayo mashabiki wake watakuwa wenye furaha ni Arsenal, ambayo inashika nafasi ya saba ikiwa na rasilimali za pauni 740m.

Chelsea, chini ya tajiri Roman Abramovich, inashika nafasi ya 46 katika orodha hiyo, ambayo timu za soka ndizo zinaongoza katika orodha zikiwamo Bayern Munich (19), AC Milan (34) na Juventus (49).

Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kuona Barcelona, ambayo kwa sasa inasemekana kuwa klabu bora duniani, ikiwa ya 26 katika orodha hiyo kwa rasilimali za pauni 606m.

Nafasi 10 za kwanza ni kama ifuatavyo:
1. Man United - Pauni 1.165bilioni
2. Dallas Cowboys- Pauni 1.13bn
3. New York Yankees- Pauni1.06bn
4. Washington Redskins- Pauni 960m
5. Real Madrid- Pauni 900m
6. New England Patriots- Pauni 850m
7. Arsenal- Pauni 740m
8. New York Giants- Pauni 734m
9. Houstan Texans- Pauni727m
10. New York Jets- Pauni 708m