Friday, July 1, 2011

vp Tanzania tukii Apply itawork? hahaha......

be the first to know..

India mbioni kudhibiti idadi ya watu

Ongezeko kubwa la idadi ya watu nchini India imewalazimu maafisa wa Afya kuanza kampeni mpya ya mpango wa uzazi.
India
Serikali inawasiwasi kuhusu idadi kubwa ya watu
Mpango huo mpya wa uzazi unanuia kuwashawishi wanawake na wanaume kukubali njia ya kumaliza kabisa nguvu za mayai ya uzazi.
Wanaokubali watapokea zawadi ya gari lipya miongoni mwa zawadi nyingine.
Tata nano, ndio gari lenya bei rahisi sana duniani lakini kulingana na kampeni hiyo, bila shaka kuna uwezekano likawa maarufu zaidi nchini India katika siku chache zijazo.
Dakatri Sitaram Sharma anatazamia kuwa huenda gari hilo likawa kishawishi tosha kwa wakazi wa jimbo la Jhunjunu kujitokeza kufungwa kizazi.
Lengo la Daktari Sharma ni kuwa jumla ya wanawake na wanaume elfu 20 watajitokeza kufungwa kizazi.
Kwa taarifa yako, gari sio zawadi tu itakayotolewa kwenye kampeni hiyo. Watakao fika watapewa piki piki, televisheni na vifaa vya kisasa vya kusagia vyakula.
Mpango huo hauja lenga tuu wakaazi wa jimbo hilo ambalo mara nyingi linakabiliwa na ukame.
Serikali ya India imekuwa ikitatizika na idadi ya raia wake ambayo inakuwa kwa kasi sana.
Hofu za utawala nchini India ni kuwa ifikiapo mwaka wa 2030, heunda idadi ya watu walioko nchini humo ikazidi ile ya wachina.
Hata hivyo hakuna uhakika kuwa kampeni hii itaungwa mkono kote nchini India.
Mwaka wa 70 ilipojaribiwa, maelfu ya watu walijotekeza kisha serikali ikashindwa kutimiza ahadi zake kitu kilicho wachukiza wengi ambao walidai kuwa serikali ilikuwa imewalaghai...

3 comments:

  1. ufisadi ni mkubwa kaka, Nchi yetu ni mali ya wachache hivyo ni vigumu kufanya jambo kama hilo. India wanahitaji maendeleo ya wananchi wake ndo maana wakafanyahivyo, but for Tanzanians, Selfishness imetawala;

    ReplyDelete
  2. mafisi ni wengi nchini kaka!!viongozi hawana uchungu wa kufanya hivyo;

    ReplyDelete
  3. ufisadi kaka, nchi yetu ni ya mafisaadi, hawana uchungu hata kidogo, wala hawana niya ya maendeleo, hivyo applicability ya sera kama hiyo ya India ni ndoto ya mchana kwetu; labda vijana 2zidi kusoma japo myanya ni midogo, si ndo wakuleta changes; eric UDSM

    ReplyDelete

please use the appropriate language to comment. Ze great respects comments from his esteemed readers. thanks for visting this blog.